Gharama za kusafisha figo kupunguzwa

0
211

Serikali ina mpango wa kupunguza gharama zinazotumiwa na wananchi katika kusafisha figo kwa kununua vifaa na vitendanishi moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji.

Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu swali la Mariam Kisangi mbunge wa viti maalum, aliyetaka kufahamu mkakati wa serikali kusaidia wagonjwa wa figo kupata matibabu ya kusafisha figo kwa gharama nafuu.

Dkt. Mollel amesema muswada wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote utakapokamilika utakuwa suluhisho la kudumu kwa wananchi wanapotaka kupata huduma ya matibabu.

“Sera ya afya ya nchi inaelekeza hakuna Mtanzania anayetakiwa kufa kwa sababu ya kukosa fedha, hivyo serikali imekuwa ikitoa msamaha kwa wasio na uwezo na waliotimiza vigezo.” amesema Dkt. Mollel