Fedha za umma zawatokea puani viongozi

0
353

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga imeokoa zaidi ya TZS 16 milioni za malipo hewa kwa watumishi wa umma katika kipindi cha mwezi mmoja.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, Christopher Maliba wakati alipokua akitoa ripoti ya robo ya pili ya mwaka 2019/2020 ambapo amebainisha kwamba bado kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya viongozi wa taasisi na mashirika ya umma kuendelea kupitisha fedha za malipo hewa jambo linalosababisha fedha nyingi za serikali kupotea.

Aidha, Kamanda Maliba amesisitiza fedha hizo kurudishwa mara moja na kuongeza kuwa hatua za kisheria zitafuata Kwa wale wote watakaobainika kuhusika ikiwemo viongozi wanaopitisha malipo hayo.