Fedha za Uhuru zijenge mabweni

0
95

Rais Samia Suluhu Hassan amefuta sherehe za maka 61 ya Uhuru na kuagiza fedha shilingi milioni 960 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hizo kuelekezwa katika ujenzi wa mabweni katika shule 8 zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, George Simbachawene ametoa taarifa leo ambapo amesema fedha hizo zitaelekezwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kusimamia ujenzi huo ili kutatua changamoto za uhaba wa mabweni katika shule hizo.

Waziri Simbachawene amesema kuwa maadhimisho ya sherehe hizo yatafanyika kwa njia ya midahalo na makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika wilaya zote hapa nchini kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka nchini ilikotoka, ilipo na inakoelekea kuhusu maendeleo endelevu ambayo Tanzania imefikia.