Faru Rajabu wa Serengeti amekufa

0
151

Faru Rajabu mwenye umri wa miaka 43 aliyekuwa akiishi katika hifadhi ya Taifa Serengeti amekufa usiku wa kuamkia hii leo kutokana na sababu ya uzee.
 
Faru Rajabu alikuwa ni mtoto wa Faru John aliyekufa mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 47.
 
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imeeleza kuwa,
Faru Rajabu ameacha watoto, wajukuu na vitukuu kadhaa.
 
Alizaliwa kwenye eneo la Ngorongoro mwaka 1979 na mwaka 1993 alihamia katika hifadhi ya Taifa Serengeti.