Fahamu chimbuko la kanisa la AICT

0
222

Kati ya mwaka 1877 hadi mwaka 1909 kanisa hilo lilikuwa likiitwa CMS yaani Church Missionary Society likiwa limeanza kazi ya kuhubiri Injili Afrika Mashariki katika maeneo ya Bagamoyo nchini Tanganyika (Sasa Tanzania).

Kuanzia mwaka 1909 hadi mwaka 1937  Peter Cameron Scott alianzisha huduma iitwayo AFRICA INLAND MISSION (AIM) huko mjini Philadelphia nchini Marekani.

Madhumuni yakuanzisha huduma hiyo yakiwa ni kuhubiri injili na kuanzisha makanisa mengine mengi katika bara la Afrika.

Kati ya mwaka 1937 hadi mwaka 1956 kanisa lilianzishwa rasmi na kupewa jina la Eklezia Evanjeli ya Kristo (E.E.K) ambapo mwaka 1957 jina la kanisa hilo lilibadilishwa na kuitwa Africa Inland Church Tanganyika (AICT) likaendelea kutumika hadi sasa.

Hadi kufikia wakati huo kiongozi mkuu wa kanisa alikuwa akifahamika kwa cheo cha Ukurugenzi na kiongozi huyo wa kwanza wa AICT alikuwa ni Mchungaji Jeremia Mahalu Kisula ambaye baadaye alikuwa Askofu wa kwanza wa kanisa hilo.

Hata hivyo jina la Ukurugenzi lilibadilishwa na kuitwa Uaskofu mnamo mwaka 1966 ambapo askofu akaendelea kuchaguliwa kila baaada ya miaka minne.

Kwa sasa kanisa la AICT linapatikana katika Dayosisi ya Pwani, Shinyanga, Mara, Ukerewe, Geita,Tabora, Mwanza na Dayosisi ya Kati.