EU kuendelea kuchangia bajeti ya Maendeleo Tanzania

0
159

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Manfred Fanti Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Balozi wa EU hapa nchini Manfred Fanti amesema mazungumzo yake na Rais Magufuli yamekuwa na manufaa makubwa ambapo wamejadili maendeleo mazuri ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na EU, na kwamba katika siku za karibuni wamekamilisha mazungumzo yaliyoruhusu kuendelea kwa mpango wa EU kuchangia bajeti ya maendeleo ya Tanzania ambapo shilingi Bilioni 132 zilizokuwa zimezuiwa zimeruhusiwa na sasa wanaandaa mpango mwingine wa miaka 7 utakaoanza mwaka huu.

Manfred Fanti amesema kwa jinsi anavyoyaona maendeleo ya Tanzania ana matumaini makubwa kuwa EU itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Tanzania ili kufanya vizuri zaidi.

Rais Magufuli amemshukuru Balozi Fanti kwa juhudi zake za kuimarisha uhusiano wa Tanzania na EU na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na EU katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa pande zote mbili.