England na Ujerumani uso kwa uso hatua ya 16 bora Euro 2020

0
241

Hatua ya makundi ya michuano ya Euro 2020, imemalizika na timu 16 zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Mechi inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya England dhidi Ujerumani, Ubelgiji dhidi ya Ureno ambazo zimeonesha kiwango bora kwenye hatua ya makundi.

Croatia nao wataumana na Hispania, Ufaransa dhidi ya Switzerland na Sweden dhidi ya Ukraine.

Nani kupenya hatua ya robo fainali?.