Elimu Ya Montessori Yapigiwa Chapuo

0
187

Kamishna wa Elimu nchini Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema elimu inayotolewa na Jumuiya ya Montessori ina manufaa kwa jamii kwa kuwa imejikita katika kuwaelimisha watoto katika umri mdogo.

Akifungua kongamano la 26 la Jumuiya ya Montessori Tanzania Dkt. Mtahabwa amesema, Jumuiya hiyo inafanya kazi kubwa katika kutoa elimu kwa watoto wa Kitanzania na kwamba wakati umefika kwa elimu hiyo kupewa kipaumbele.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya ya Montessori Sarah Kiteleja amesema, mazingira ya Montessori yanamwandaa mtoto tangu anapozaliwa hadi umri wa miaka 6 na wanalindwa na kupata elimu bora.