Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali imeanza mchakato wa Katiba mpya kwa kuandaa bajeti ya elimu ya Katiba, iliyopitishwa katika bunge la bajeti lililopita.
Dkt. Ndumbaro amesema kasma ya fedha ya Katiba itaendelea kuboreshwa mwezi Desemba mwaka huu.
Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema elimu hiyo itaanza kutolewa rasmi mwezi Septemba mwaka huu ambapo mchakato huo utakuwa unatolewa na asasi za kiraia, viongozi wa dini na wasomi wa vyuo vikuu.
Dkt. Ndumbaro alikuwa akizungumza mkoani Ruvuma, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.