Eid kusherehekewa Jumatatu au Jumanne

0
249

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewatangazia Waislamu na Watanzania wote kuwa Sikukuu ya Eid El Fitr itakuwa siku ya Jumatatu Mei 02, 2022 au Jumanne Mei 03, 2022 kutegemea kuandama kwa mwezi.

Sherehe za Eid kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika mkoani Dar es Salaam ambapo swala ya Eid itaswaliwa msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA makao makuu Kinondoni kuanzia saa 1:30 asubuhi.

Baraza la Eid litafanyika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 8 mchana.