Ebola yaibuka upya DRC

0
228

Mwanaume mmoja raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) amefariki dunia baada ya kupata maambukizi ya Ebola, ikiwa ni miezi minne tangu Jamhuri hiyo ishambuliwe tena na ugonjwa huo.

Aprili 5 mwaka huu mwanaume huyo aliwekwa chini ya uangalizi maalum huku akipatiwa matibabu lakini hali haikuwa nzuri na hivyo kufariki dunia.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti amesema, “Wakati hauko upande wetu, ugonjwa umeanza kwa wiki mbili na sasa tunapaswa kukimbizana nao.”

Hadi sasa watu 70 waliokuwa karibu na Mwanaume huyo wamewekwa chini ya uangalizi maalum ili kubaini endapo wana maambukizi ama la.

DRC ni nchi ambayo ina uzoefu mkubwa katika kupambana na ugonjwa wa Ebola, kwani huu ni mlipuko wa 14 kwa nchi hiyo tangu ulipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 1976.