Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana katika kulinda rasilimali za maliasili za nchi hizo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadaye.
Waziri Chana ameyasema hayo katika mkutano wa 10 wa Baraza la Kisekta la Usimamizi wa Mazingira na Maliasili la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha.
Akifungua mkutano huo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Veronica Nduva amesema majadiliano ya mkutano huo yalijikita katika kukuza ushirikiano na kuimarisha mifumo ya kusimamia na kulinda maliasili zilizopo katika ukanda wa Afrika Mashariki.