Dorothy Semu amrithi Zitto ACT

0
590

Chama cha ACT – Wazalendo kimemchagua Dorothy Semu kuwa kiongozi wa chama hicho akimrithi Zitto Kabwe ambaye muda wake umemalizika.

Dorothy amechaguliwa katika mkutano mkuu wa ACT – Wazalendo uliofanyika mkoani Dar es Salaam Machi 06, 2024.

Kabla ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo kwa upande wa Bara.

Pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho na
Katibu wa Sera na Utafiti wa ACT – Wazalendo.