Dola Mil 5 kuwekezwa hospitali ya Tanzanite

0
244

Kampuni ya ES Healthy Care Centre ya nchini india inayojishughulisha na masuala ya afya ina mpango wa kuwekeza Dola Milioni tano za Kimarekani
kwa ubia na hospitali ya Tanzanite iliyopo jijini Mwanza.

Hayo yamebainika wakati ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika katika ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) mkoani Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na maafisa wa kituo hicho.

Ujumbe huo kutoka kampuni ya ES Healthy Care Center umefika nchini baada ya uongozi wa hospitali ya Tanzanite kufanya ziara nchini India kwa lengo la kutafuta
Wawekezaji kupitia ziara ya utalii wa matibabu iliyoratibiwa na TIC.

Mkataba wa makubaliano kati ya pande hizo mbili tayari ulisainiwa nchini india.

Fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha dawa za binadamu, ujenzi wa kituo cha mafunzo ya afya na maboresho ya miundombinu ya hospitali hiyo ya Tanzanite ya jijini Mwanza.