Vitabu 4,000 vyasambazwa shuleni Dodoma

0
153

Changamoto ya kushika nafasi za mwisho katika sekta ya elimu kwa mkoa wa Dodoma imeanza kutatuliwa baada ya wadau wa elimu kuanza kushirikiana kuondoa aibu hiyo.

Vitabu zaidi 4,000 vyenye thamani ya shilingi milioni 27 vimetolewa na shirika lisilo la kiserikali la
Africa Proper Education Network kuziwezesha shule za msingi na sekondari kupata vitabu vya kiada lengo likiwa ni kusaidia kuinua kiwango cha elimu mkoani humo.

Akitoa vitabu hivyo Hermes Damiani amesema kuwa shirika la hilo limetoa vitabu vya aina mbalimbali 58 kwa kuzingatia umuhimu wa vitabu hivyo kwa wanafunzi wa ngazi ya shule ya msingi na sekondari.

“Serikali itambue mchango wa wachapishaji binafsi wa vitabu ili kuweza kufanikisha ufanisi wa ubora wa elimu nchini,” amesisitizs Damiani

Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Dodoma, Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Nathalis Linuma, amesema vitabu hivyo vitafungua ukurasa mpya wa wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao