Dodoma: Rais Magufuli aahirisha sherehe za mashujaa

0
421

Rais wa Tanzania, John Magufuli ameahirisha sherehe za Mashujaa zilizopaswa kufanyika Julai 25, 2020 jijini Dodoma.

Pamoja na kuahirisha sherehe hizo, Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kutumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwaombea Mashujaa wote waliojitoa kwa ajili ya nchi yetu na hata wale ambao wametoa mchango mkubwa katika ngazi mbalimbali zikiwemo mtu mmoja mmoja na familia.

Rais Magufuli amewatakia heri Watanzania wote kuelekea siku hiyo na amewataka kuendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano.