Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema Serikali itahakikisha inawasaidia Wanawake katika nyanja zote.
Akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa upande wa Zanzibar Dkt. Mwinyi amesema, Wanawake hawataachwa nyuma katika masuala ya kiuchumi pamoja na nafasi mbalimbali za uongozi.
Amesema atahakikisha akiwa madarakani ataongeza idadi ya Wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi Serikalini pamoja na kwenye siasa.
Ameongeza kuwa atahakikisha anaboresha huduma mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na afya na elimu, maana kwa kufanya hivyo kutasaidia kuendelea kumkomboa Mwanamke.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Zanzibar ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni zingatia usawa wa kijinsia kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa maisha endelevu.