Dkt. Stergomena Tax ateuliwa kuwa Mbunge

0
143

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt. Tax ameteuliwa kutoka kwenye nafasi kumi za Wabunge wa kuteuliwa na Rais.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Tax alikuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye amemaliza muda wake mwezi Agosti mwaka huu.

Mbunge huyo ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.