Dkt Shoo kuiongoza KKKT kwa kipindi cha pili

0
268

Askofu Fredrick Shoo kutoka Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amechaguliwa kuwa Mkuu wa kanisa hilo kwa kipindi kingine cha pili.

Dkt Shoo amechaguliwa kushika wadhifa huo, wakati wa uchaguzi uliofanyika mkoani Arusha baada ya kupata kura 144 kati ya kura zote 218 zilizopigwa.

Wagombea wawili walikua wakiwania nafasi hiyo, ambpo Askofu Abernego Keshomshahara kutoka Dayosisi ya Kaskazini Magharibi amepata kura 74.

Dkt Shoo ataliongoza Kanisa hilo la KKKT kwa kipindi cha Pili ambacho kitakua ni cha miaka Minne.