Dkt. Semesi ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu NEMC

0
293

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Immaculate Semesi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Semesi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu ambapo anachukua nafasi ya Dkt. Samuel Mafwenga ambaye amemaliza muda wake.