Rais Samia Suluhu Hassan ametangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa baada ya kupata kura 1914 kati ya kura 1915 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa 10 wa CCM unaofanyika mkoani Dodoma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa upande wa Zanzibar.
Rais Mwinyi amepata kura 1,912 kati ya kura zote 1,915 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa 10 wa CCM.
Abdulrahman Kinana ametangazwa mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, baada kupata kura zote 1,915 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa 10 wa CCM unaofanyika mkoani Dodoma kwa muda wa siku mbili.
Kabla ya uchaguzi huo, Kinana alikuwa akihudumu katika nafasi hiyo hiyo.