Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayub Rioba ametoa wito kwa Waandishi wa habari nchini kusoma vitabu na nyaraka muhimu ili kusimamia, kulinda mabadiliko na maslahi ya Taifa dhidi ya mabeberu.
Dkt Rioba ametoa wito huo jijini Dar es salaam wakati wa mdahalo maalum wa kukabidhi kitabu kinachojulikana kama Nguli wa Utangazaji, kilichoandikwa na mwandishi wa TBC, – Teonas Aswile.
Amesisitiza kuwa, Waandishi wa habari nchini wanapaswa kuelewa na kusimamia muelekeo salama wa Taifa.
Wakati wa mdahalo huo maalum uliofanyika kwenye Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC), washiriki pia wamepata fursa ya kutazama dhana iliyopo katika kitabu hicho.
Kwa mujibu wa Dkt Rioba, Aswile ameweka kumbukumbu muhimu kwenye tasnia ya Utangazaji nchini kwa kuandika kitabu hicho cha Nguli wa Utangazaji.