Dkt. Nchimbi asimikwa Chifu wa Wapare

0
164

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani humo.

Kabla ya mkutano huo Dkt. Nchimbi alisimikwa kuwa Chifu wa Kabila la Wapare.

Katika ziara hiyo mkoani Kilimanjaro Dkt. Nchimbi ameongozana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makalla, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia Hamid Abdallah pamoja na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Ussi Gavu.

Baadae hii leo, Katibu Mkuu wa CCM na ujumbe wake atawasili mkoani Tanga kwa ajili ya kuhitimisha ziara yake katika mikoa mitano ambapo mingine ni Singida, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.