Dkt Mwinyi : Zanzibar tunajivunia maisha ya Mzee Mkapa

0
152

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema, uongozi wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania Hayati Mzee Benjamin Mkapa umeacha alama kubwa katika maisha ya Wananchi wa Zanzibar.

Akihutubia Kongamano la Kumbukizi ya mwaka mmoja baada ya kifo cha Mzee Mkapa, Dkt. Mwinyi amesema wakati wa uongozi wake Rais Mkapa alisimamia upatikanaji huduma bora kwa Wananchi wote ikiwa ni pamoja na wale wa Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amesema, Hayati Rais Mkapa alisimamia Muungano kwa nguvu kubwa na hakutetereka, na hilo ni jambo kubwa la kukumbukwa na Wananchi wa pande zote mbili.

Amesema, Hayati Mkapa alikuwa Kiongozi mwenye maono na upendo mkubwa, na aliyeamini katika kuwatumikia Wananchi hasa wanyonge na wanaoishi maeneo ya pembezoni.