Rais wa Zanzibar na Mwenuyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alikuwa kiongozi aliyechukia uonevu na muadilifu kwa jamii aliyoiongoza hatua ambayo imesababisha kupigania uhuru wa nchi za Bara la Afrika
Dkt. Hussein Mwinyi ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kumbukizi ya miaka 100 tangu kuzaliwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kumbukizi ambayo imefanyika Msasani mkoani Dar es Salaam.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majliwa amesema Watanzania wataendelea kumkumbuka na kuyaenzi yale yote mazuri yaliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na uongozi wake utaendelea kuenziwa ikiwemo kuimarisha misingi ya utawala bora