Dkt Mwinyi kupeperusha bendera ya Urais CCM Zanzibar

0
307

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais John Magufuli amemtangaza Dkt Hussein Mwinyi kuwa ndio mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Dkt Mwinyi ameshinda baada ya kupata kura 129 ambazo ni sawa na asilimia 78.65 ya kura zote zilizopigwa na wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM katika kikao kinachoendelea hivi sasa jijini Dodoma.