Dkt.Mwinyi azindua mfumo wa kieletroniki wa uwekezaji

0
122

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi amesema lengo la Serikali ni kuimarisha na kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara katika uwekezaji hapa nchini.

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo wakati akizindua Muongozo wa Uwekezaji na Mfumo wa Kieletroniki wa Uwekezaji, wenye lengo la kurahisisha utoaji huduma kwa wawekezaji ikiwemo usajili na upatikanaji wa cheti cha uwekezaji wenye jina la “ZANZIBAR INVESTMENT ELECTRONIC WINDOW” (ZieW).

Ameongeza kuwa kukuza uwekezaji na kuleta maendeleo ni moja ya malengo makuu ya Serikali.