Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amewataka wakazi wote wa Zanzibari kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika hapo kesho.
Dkt. Mwinyi ametoa wito huo katika hafla ya makabidhiano ya anuani za makazi, iliyofanyika katika makazi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Migombani mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema serikali imefikia uamuzi wa kuifanya tarehe 23 mwezi huu kuwa ya mapumziko, ili kutoa fursa kwa wananchi wote kuweza kushiki kikamilifu katika zoezi hilo litakalofanyika nchini kote.
“Mimi nitashiriki zoezi hilo na matumaini yangu Wazanzibari wote watashiriki na kumalizika kwa salama na amani.” amesema Rais Mwinyi