Dkt. Mwinyi Atengua utezi wa Katibu wake

0
182

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Katibu wa Rais Suleiman Ahmed Saleh.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Dkt. Abdulhamid Mzee imesema kuwa maamuzi hayo ya Rais yameanza leo Tarehe 14 Disemba 2020.

Taarifa hiyo imesema kuwa uamuzi hio wa Rais Mwinyi imetokana na uwezo aliopewa na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 12(3) cha sheria ya utumishi wa umma namba 2 ya mwaka 2011.