Dkt.Mwinyi atengua uteuzi wa viongozi mbalimbali

0
222

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Mwinyi leo Februari 3, 2022 ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said imeeleza, Dkt. Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Idara ta Utumishi na Uendeshaji katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Omar Ali Omar.

Pili, Dkt.Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Tasisi ya Elimu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Suleiman Yahaya Ame.

Tatu, Rais Mwinyi ametengua uteuzi wa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Fatma Iddi Alli.

Nne, Rais ametengua uteuzi wa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Fatma Iddi Alli.

Tano, Dkt.Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Watoto katika Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto