Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu Dkt. Charles Msonde amewataka walimu kutumia kanuni ya kuchunguza uwezo wa mwanafunzi na watumie nyezo zitakazomwezesha mwanafunzi kuelewa vizuri badala ya kuharakisha kumaliza mada.
Dkt. Msonde amesema hayo wakati akizungumza na walimu wa shule mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Amesema ni bora mwanafunzi akafundishwa na kuelewa vizuri hata mada 15 kuliko kumharakisha kumfundisha ili umalize mada 20 na asielewe.
Dkt. Msonde amesema walimu wana wajibu wa kurekebisha makosa ya walimu wengine huko nyuma katika masomo ili kumsaidia mwanafunzi kuelewa masomo vizuri.