Dkt. Mpango kwenda Mtwara

0
199

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, tarehe 23 mwezi huu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Mtwara.

Akiwa mkoani Mtwara pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais atashiriki kwenye Misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mzee Benjamin Mkapa, itakayofanyika katika kijiji cha Lupaso wilayani Masasi.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewaambia Waandishi wa habari mkoani Mtwara kuwa, Dkt. Mpango pia atafungua soko la kisasa la Jida lililoko wilayani Masasi, atazungumza na Wananchi wa Masasi,; pamoja na kufungua kiwanda cha kubangua korosho cha wilaya ya Newala.

Akiwa wilayani Mtwara, ataweka jiwe la msingi katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, ambayo imejengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 15.