Dkt. Mpango kushiriki jukwaa la usawa

0
216

Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) linaanza hii leo huko Paris nchini Ufaransa.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ambaye tayari yupo jjjini Paris, anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika jukwaa hilo.

Jukwaa hilo la Kizazi cha Usawa lina lengo la kuchagiza haki za usawa wa kijinsia kama zilivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing wa mwaka 1995.

Akiwa nchini Ufaransa, Dkt. Mpango amepata maelezo kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini humo Samwel Shelukindo ya namna ubalozi huo unavyotekeleza sera ya Diplomasia ya Uchumi katika eneo lake la uwakilishi ambalo ni Ufaransa, Hispania, Ureno, Algeria na Morocco.

Dkt. Mpango amemtaka Balozi Shelukindo kuendelea kushirikiana na sekta binafsi zilizopo nchini Ufaransa kwa manufaa ya pande zote mbili.