Dkt. Mpango kumuwakilisha Rais SADC

0
205

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anaondoka nchini hii leo kuelekea Lilongwe, Malawi kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 12 mwezi huu.

Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama utakaofanyika tarehe 11 mwezi huu.