Dkt. Mpango kuhutubia jukwaa la Kizazi chenye usawa

0
227

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango leo anatarajiwa kutoa ahadi za Tanzania katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa linalofanyika huko Paris nchini Ufaransa.

Dkt. Mpango anatoa ahadi hizo katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaonekana kama kinara wa uwezeshaji Wanawake kiuchumi kama ilivyoridhiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Jukwaa hilo lenye madhumuni ya kuchagiza usawa wa kijinsia, linajadili umuhimu wa uwezeshaji Wanawake kiuchumi kama nyenzo ya kumnyanyua Mwanamke kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Mengine ni kumwezesha Mwanamke kupata Teknolojia rahisi na sahihi katika kufanya shughuli za kiuchumi, kutolewa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na utoaji wa mitaji kwa Wanawake pamoja uwepo wa mifumo sahihi ya kidigitali katika shughuli za kiuchumi zinazofanywa na Wanawake.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika jukwaa hilo.