Dkt. Mpango : Kuandika Wosia si kujitabiria kifo

0
153

Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango amewasihi Watanzania kujijengea tabia ya kuandika Wosia ili kujiepusha na migogoro ya mali na kifamilia kinapotokea kifo huku akisisitiza kuwa kufanya hivyo haimaanishi mtu huyo yuko mbioni kufariki dunia.

Ameiagiza wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Wosia na masuala ya mirathi kwa ujumla.

“Hakuna ajuae siku ya kufa, lakini ukweli ni kwamba sisi wote tutakufa. Migogoro mingine ya mirathi inatokana na fikra potofu kuwa Mke wa marehemu hana haki ya kurithi mali zilizopatikana wakati wa uhai wa Mume wake,” ameeleza Dkt. Mpango.