Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka Watanzania kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira.
Amesema utunzaji na uhifadhi wa mazingira ni muhimu, kwani uharibifu wa mazingira hayo limekuwa tatizo lenye athari mbaya kwa Taifa na dunia.
Kwa upande wa serikali Dkt. Mpango amesema itachukua hatua kali kwa yeyote atakayejihusisha na uharibifu wa mazingira ikiwa ni.pamoja na kuchoma moto misitu na kuharibu vyanzo vya maji.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wilayani Kasulu mkoani Kigoma,
aliposhiriki misa takatifu ya Upadirisho wa mapadre sita wa kanisa Katoliki jimbo la Kigoma iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Luka kwenye kijiji cha Makere.
Amewataka mapadre hao kujiepusha na sababu zozote za kulaumiwa pamoja na kushtakiwa kama yasemavyo maandiko katika biblia.
Akiwa kanisani hapo, Makamu wa Rais amechangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Luka.