Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi Duniani (GCA) Profesa Patrick Verkooijen.
Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29), unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya Tanzania na taasisi hiyo katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Wengine walioshiiriki mazungumzo hayo ni pamoja na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Ashatu Kijaji na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Hussein Katanga.