Dkt. Mollel : Tuwasaidie wawekezaji wa bidhaa za Afya badala ya kuweka vikwazo

0
282

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa mamlaka na taasisi zinazosimamia bidhaa za afya ikiwemo Dawa, vifaa tiba pamoja na vitendanishi kuwasaidia Wafanyabiashara wa bidhaa hizo kufanya biashara kwa mujibu wa Sheria na taratibu badala ya kuwa vikwazo ili wananchi wanufaike na bidhaa hizo kwa gharama nafuu na kwa ubora unaotakiwa.

Dkt. Mollel ametoa wito huo mkoani Dar es Salaam, alipofungua mkutano wa wawekezaji wa bidhaa za dawa na Wafamasia, wenye lengo la kuwakutanisha Wafanyabiashara hao ili kujadili changamoto zao na mbinu mbalimbali za kuboresha upatikanaji wa bidhaa za dawa zenye ubora na kwa gharama nafuu kwa wanachi.

“Najua wapo baadhi ya Wataalamu wetu hawana jicho la kibiashara, wengi wanaambiwa Wasaidie watu kufanya biashara wao wanageuka polisi badala ya kuwa wasaidizi ili kuwasaidia wafanyabiashara, wengi wanakaa ofisini tu badala ya kumsaidia mfanyabiashara aanzishe biashara yeye anaangalia kasoro tu.”-amesema Dkt. Mollel

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania Fadhili Hezekia amesema maonesho hayo ya pili ya Wafamasia ni maonesho mahususi ya huduma za afya kwa Sekta nzima yanayotoa fursa kwa Watanzania kupata huduma mbalimbali za afya katika maonesho hayo.