Dkt. Magufuli aahidi kumaliza kero za wananchi wa Shinyanga

0
252

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amesema iwapo wananchi wa Mwigumbi mkoani Shinyanga watampa ridhaa ya kuongoza kipindi cha pili atahakikisha anamaliza kero za wachimbaji wadogo wadogo wa madini, miundombinu na sekta ya kilimo.

Akizungumza katika kampeni mkoani Shinyanga Dkt. Magufuli amewataka wananchi kufanya tathmini ya maendeleo yaliyofanywa na CCM tangu kipindi cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Aidha Mgombea huyo amezungumza na wananchi Maswa mkoani Simiyu katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda ikiwa ni mwendelezo wa kampeni zake.