Dkt. Magufuli aahidi kumaliza kero za ardhi

0
330

Akiomba ridhaa ya Watanzania kuongoza kwa muhula wa pili, mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amesema serikali ya awamu tano imefanikiwa kuvipatia huduma muhimu ya umeme vijiji zaidi ya 9,570 kati ya vijiji 12,170 vilivyopo nchini.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza Dkt. Magufuli amewaomba wakazi wa Mwanza kuchagua madiwani, wabunge na Rais kutoka CCM ili kukamilisha vijiji vilivyobaki vikiwemo vijiji vitano vilivyopo mkoani humo.

Kuhusu changamotoo za ardhi, Dkt. Magufuli amesema iwapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuongoza serikali katika kipindi cha miaka mitano ijayo, watarasimisha nyumba za wakazi wanaoishi milimani ili kuwaondolea adha ya kubomolewa.

Pia amesema serikali imejipanga kuongeza ndege nyingine tano ikiwemo ndege kubwa moja ya mizigo na kutenegeneza ajira milioni 8.