Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula amezitaka halmashauri ama vijiji kuhakikisha inatenga maeneo ya uwekezaji na kuyakatia hati ili kuondoa usumbufu kwa wawekezaji wanapotafuta ardhi ya kuwekeza.
Dkt. Mabula ametoa rai hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa wa Mbeya, na kuwataka wakurugenzi na wasimamizi wa ardhi katika maeneo yao kuhakikisha wanayakatia hati maeno yaliyotengwa kwa uwekezaji.
Ameongeza kuwa mara kadhaa wawekezaji wamekuwa wakipata usumbufu wa kutafuta vibali vya maeneo ya uwekezaji na hivyo kuchelewesha kazi ya uwekezaji hapa nchini.
Aidha amezitaka ofisi ya ardhi katika mkoa wa Mbeya kushirikiana na Halmashauri pamoja na Vijiji kupima na kuyapatia hati maeneo ya uwekezaji mkoani humo.