Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema wizara hiyo inaendelea kufuatilia taarifa za uwepo wa jiwe kubwa la madini aina ya ruby, lililovunja rekodi kwenye soko la madini katika Falme za Kiarabu.
Dkt. Kiruswa ameliambia Bunge jijini Dodoma kuwa wanafuatilia jambo hilo
ili kupata uhakika,
japo taarifa zinaonesha mmiliki wa jiwe hilo yupo nchini Marekani.
Jiwe hilo la Ruby lenye uzito wa kilo 2.5 lina thamani ya dola milioni 120 za Kimarekani katika soko.