Dkt Kikwete ataka Tanzania kujitangaza kupitia AGRF

0
290

Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amesema, huu ni wakati muafaka kwa Tanzania kuitumia fursa ya kujitangaza duniani kupitia mkutano wa Afrika wa masuala ya Chakula na Kilimo (AGRF) unaotarajiwa kufanyia nchini mwezi Septemba mwaka huu.

Dkt. Kikwete ameyasema hayo Ikulu, Dar es Salaam, wakati wa
mkutano wa maandalizi ya mkutano huo wa AGRF, uliohudhuriwa na Viongozi na wageni mbalimbali, pamoja na Wadau wa sekta ya kilimo na chakula.

Amesema mkutano huo wa
AGRF ni fursa kwa Tanzania kuitangazia Dunia kuwa inaweza kujiimarisha katika kilimo na kusaidia Afrika kujiimarisha katika sekta hiyo na kuwa na uhakika wa chakula.

Rais Mstaafu Kikwete ameongeza kuwa ni muhimi kuwakumbuka zaidi Wanawake na Vijana kwenye fursa zitakazopatikana kutokana na mkutano huo ili kuwasaidia kukua kiuchumi.