Dkt. Bashiru afika Zanzibar kujitambulisha

0
151

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi amempongeza Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Balozi Dkt Bashiru Ally
kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Rais Dkt Mwinyi ametoa pongezi hizo alipofanya mazungumzo na Dkt Bashiru aliyefika Ikulu jijini Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha.

Rais Mwinyi ameeleza kuwa yeye pamoja na viongozi wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wataendelea kumpa ushirikiano Dkt Bashiru ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Amesema Watanzania wana imani kubwa kwa Dkt Bashiru kutokana na uchapakazi wake, hivyo ni vema akapatiwa ushirikiano unaostahili ili aweze kudhihirisha jambo hilo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Dkt Bashiru Ally amemweleza Rais Dkt Mwinyi kuwa anategemea kupata ushirikiano kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na viongozi wake.

Ameahidi kuendeza ushirikiano kati yake na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said, lengo likiwa ni kuhakikisha shughuli zote zinafanyika kama ilivyokusudiwa.

Kabla ya kukutana na kufanya mazingumzo.na Rais Mwinyi, Dkt Bashiru alikutana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said Ikulu jijini Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao waliahidi kuimarisha ushirikiano na kuendelea kuratibu shughuli zao kwa ushirikiano.