Dkt. Ashatu: Tuzalishe malighafi zetu

0
148

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ametoa wito kwa Watanzania kuongeza kasi na uwezo wa kuzalisha bidhaa kwa kutumia malighafi zinazozalishwa nchini.

 Dkt. Kijaji ametoa wito huo mkoami Dar es Salaa wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari la 600 lililoundwa na kiwanda cha GF Trucks and Equipment LTD kilichotimiza miaka 15 tangu wa kuanzishwa kwake, halfa iliyofanya wakati wa maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa maarufu sabasaba yanayoendela hivi sasa.
 
Amesema sasa ni wakati wa kuchangamkia fursa zilizopo katika Eneo Huru la Biashara Afrika, kwani Tanzania ilikuwa katika majadiliano ya makubaliano ya asilimia 20 ya malighafi za uundaji wa magari kuwa zinazalishwa nchini au Afrika.
 
Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kuwa waaminifu katika soko kwa kuhakikisha alichoagiza mteja ndicho anachopokea, ili wateja wa ndani na nje wawe na imani na soko la Tanzania.