Dkt. Ashatu : Hatutaagiza tena sukari toka nje

0
263

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema mpaka kufikia mwaka 2023, Tanzania haitaagiza tena sukari kutoka nje.

Dkt. Ashatu ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliokua na lengo la kuangazia hali ya uchumi wa Taifa pamoja na kupanda kwa bei za bidhaa nchini, mkutano ambao pia umemshirikisha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba.

“Ni lengo la Serikali na hili tutalisimamia ipasavyo kwamba mpaka kufika mwaka 2023 hatutakuwa na ‘gape’ la sukari tena, hatutaagiza tena sukari kutoka nje tutakuwa na sukari inayojitosheleza, tunasema haya tayari tuna Wawekezaji na viwanda vyetu vinatanuka.” amesema Waziri huyo wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Amesema uamuzi huo umetokana na changamoto ya uhaba wa sukari nchini na kwamba tayari Serikali imeweka mazingira mazuri ili viwanda vyote viwe katika mpango wa kuongeza uzalishaji wa sukari.