Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amevitaka vyombo vya habari nchini kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maadili yanayoongoza tasnia hiyo, ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.
Dkt. Abbasi ametoa rai hiyo jijini Dodoma wakati akitoa mada kwenye mafunzo yaliyowashirikisha Waandishi wa habari za mtandaoni wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) (Tbconline).
Amesema chombo cha habari A kinapotumia taarifa ya habari ya chombo B ni lazima kieleze kuwa taarifa hiyo imetolewa na chombo A.
Aidha, Dkt. Abbasi ameongeza kuwa ni kosa kisheria kwa chombo chochote cha habari kutumia kazi ya chombo kingine bila kusema au kuhariri kazi ya awali ili kuuaminisha umma kuwa kazi hiyo ni yake.
Amewasihi Waandishi wa habari nchini kujisomea na kufanya tafiti, kwani kazi wanayofanya ni kubwa na imebeba mustakabali wa maendeleo ya Taifa.