Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga na ujumbe wake kwa mazungumzo Ikulu Zanzibar tarehe 05 Desemba 2023.
Zanzibar kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Tathmini ya muda wa kati wa mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia(IDA20 Mid Term Review) unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023 katika hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar ukiwashirikisha wajumbe zaidi ya 3,000 kutoka mataifa takribani 100 duniani.
Rais Dk.Mwinyi ataufungua mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.
🗓️05 Desemba 2023
📍Ikulu Zanzibar