Mtangazaji wa kipindi cha Papaso cha TBC FM D’jaro Arungu almaarufu Baba Mzazi, amejinyakulia tuzo ya mtangazaji bora wa Redio Afrika katika usiku wa Zikomo huko Lusaka, Zambia.
Tuzo za kimataifa za Zikomo hutolewa kwa watu ama taasisi zinazofanya vizuri zaidi kwenye maeneo yao kama uandishi wa habari, sanaa na ujasiriamali.